Watu 36 wamefariki dunia na wengine
wapatao 70 kujeruhiwa kufuatia msururu wa magari kugongana nchini
Peru baada ya basi moja kuteleza na kuingia katika njia ya upande wa
pili.
Basi hilo la Murga Serrano line,
lilijikuta likigongwa na magari matatu madogo yaliyokuwa yakitoka
upande wa pili, na kisha kugongwa pia na mabasi mengine mawili na
lori moja.
Basi hilo lilikuwa limebeba ujumbe
wa waumini wa taasisi ya kikristo ya Wamishonari wa shirika la
Worldwide Missionary Movement.
Muonekano kwa mbele wa basi hilo baada ya kupata ajali



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni