Serikali ya Marekani itatoa zawadi
ya dola milioni 20 kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazofanikisha
kukamatwa viongozi wakuu wa kundi la dola ya Kiislama (IS).
Taarifa hiyo imewataja viongozi hao
wanaotafuta kuwa ni Abd al-Rahman Mustafa al-Qaduli, Abu Mohammed
al-Adnani, Tarkhan Tayumurazovich Batirashvili pamoja na Tariq
Bin-al-Tahar Bin al Falih al-'Awni al-Harzi.
Viongozi hao wanaungana na orodha ya
fungu la zawadi nono kwa watu wanaotafutwa kwa ajili ya kufikishwa
mbele ya vyombo vya dola. Hapo jana IS walisema ilihusika na
shambulio lililotokea Texas.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni