Kikosi cha wanamaji cha Italia
kimesema kimewaokoa wahamiaji 52 kutoka katika boti ya kujaza upepo
liyokuwa ikizama katika bahari ya Mediterranean huku wengine 50
hawajulikani walipo.
Meli ya kivita imefanikiwa kuwaopoa
nusu ya wahamiaji waliokuwemo kwenye boti hiyo, huku watu wengine
wawili wakiokolewa baada ya kuonekana wakining'inia kwenye pipa.
Wakati huo huo wahamiaji haramu
wameendelea kuwasili kwenye kisiwa cha Ugiriki cha Kos, ambako
kumekuwa na hofu kutokana na ongezeko hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni