Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika
nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) Babacar Gaye amefukuzwa kazi
kufuatia matukio maradufu ya udhalilishaji wa kingono yaliyofanywa na
walinda amani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki-moon amewaambia waandishi wa habari umoja huo umeomba barua yake
ya kujiuzulu.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku
moja tu kupita tangu shirika la Amnesty International kudai kuwa
mtoto wa kike wa miaka 12 alibakwa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.
Kikosi cha wanajeshi 10,000 cha
Umoja wa Mataifa kiliwekwa CAR mwaka jana kujaribu kurejesha utulivu,
lakini sasa kinakabiliwa na tuhuma za kufanya ukatili wa kingono kwa
watoto wa mitaani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni