Chama cha Taifa cha Walimu Kenya
(KNUT) kimewataka walimu wakuu kuwarejesha nyumbani wanafunzi na
kuzikabidhi shule kwa bodi za magavana, wakati vyama vya walimu
vikihimiza mgomo wao kuendelea hadi hapo watakapolipwa nyongeza ya
mshahara.
Kamati ya Kuu ya KNUT imetoa kauli
hiyo, wakati Chama cha Elimu ya Awali ya Msingi (Kuppet) kikiwataka
viongozi wakuu kuachia madaraka yao kwa kushindwa kulipa mshahara wa
walimu kwa maagizo ya mahakama.
Kwa upande wake kionngozi wa
muungano wa Cord Raila Odinga amemsihi rais Uhuru Kenyatta kuongea na
walimu juu ya namna atakavyoweza kuwalipa mishahara yao mipya badala
ya kusema serikali haina fedha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni