Vikosi vya ulinzi nchini Misri
vimewauwa kimakosa watu 12, wakiwemo watalii kutoka Mexico wakati wa
operesheni ya kukabiliana na magaidi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa
nchi hiyo amesema.
Taarifa ya wizara hiyo imesema
watalii hao walikuwa wakisafiri kwa gari lililoingia katika eneo
linalozuiwa huko Wahat katika eneo la Jangwa la Magharibi.
Watalii kumi kutoka Mexico na raia
wa Misri wamejeruhiwa katika tukio hilo na wametibiwa kwenye
hospitali moja katika eneo hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni