Kiwango kizuri katika mechi yake ya
kwanza na Manchester United alichoonyesha kinda Anthony Martial
kimewapa mashabiki kitu ambacho hawajawahi kukiona katika miaka
miwili iliyopita kwa mujibu wa mshambuliaji wa zamani mkongwe wa timu
hiyo Dwight Yorke.
Kocha Louis van Gaal alimuingiza
dimbani mchezaji huyo aliyemnunua kwa paundi milioni 36 katika
kipindi cha pili na kufunga goli lake la kwanza na timu hiyo
alilolipachika wavuni kwa kupasua ngome ya ulinzi ya Liverpool na
kumtungua kipa Simon Mignolet.
Yorke amesema Manchester United
ilikuwa inakosa mshambuliaji anayeweza kupasua katika msitu wa mabeki
na kufunga, lakini Anthony ambaye mashabiki walikuwa hawatarajii
jambo kubwa kutoka kwake alionyesha uwezo wake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni