Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) limeonya kuwa maelfu ya wakimbizi
wataachwa njia panda kufuatia nchi za Umoja wa Ulaya kuamua kutumia
sheria tofauti za kudhibiti mipaka ili kukabiliana rekodi ya idadi
kubwa ya wahamiaji.
Kauli hiyo ya UNHCR imekuja wakati
Ujerumani ikianzisha udhibiti katika mpaka wake na nchi ya Austria.
Shirika hilo limetoa wito wa
kuanzishwa kwa kituo kikubwa cha Umoja wa Ulaya cha kuwapokea
wahamiaji wanaowasili mataifa ya Ulaya.
Wakati huo huo Mawaziri wa Mambo ya
Ndani wa Ulaya, wanafanya mkutano wa dharura hii leo kujadili namna
ya kukabiliana na mgogoro wa wahamiaji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni