Gavana wa California ametangaza hali
ya tahadhari baada ya moto mkubwa kulazimisha maelfu ya watu kukimbia
nyumba zao kaskazini mwa jimbo hilo.
Gavana Jerry Brown amesema moto huo
umeteketeza nyumba katika kaunti za Napa na Lake na kutishia mamia ya
nyumba nyingine.
Zaidi ya watu 1,300 wamekimbia
makazi yao huko Middletown, kaskazini mwa San Francisco, wakati
nyumba zao zikiteketea kwa moto. Askari wanne wa zimamoto waliougua
moto mno wanapatiwa matibabu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni