Idadi ya kesi za uhalifu
ulizofanyika wakati wa sherehe za mwaka mpya katika jiji la Cologne
nchini Ujerumani zimeongezeka na kufikia 516, huku asilimia 40 zikiwa
znahusiana na mashambulizi ya ngono.
Polisi wa Jiji la Cologne wamesema
idadi ya kesi zimeongezeka kutoka 379, huku wengi wa watuhumiwa
waliotenda uhalifu huo wakidaiwa kuwa ni wahamiaji kutoka nchi za
Afrika ya Kaskazini.
Uhalifu huo umeibua ukosoaji wa sera
za Kansela Angela Merkel kufungua milango ya Ujerumani kwa ajili ya
kuwapokea wahamiaji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni