Sheria mpya zinazohitaji viongozi wa
dini Kenya kuwakilisha vyeti vya utendaji mzuri wa masula ya kiroho
pamoja na vyeti vya mafunzo ya theolojia zimekamilika tayari kwa
utekelezaji.
Sheria za Jamii na Dinia
zilizochapishwa na Ofisi ya Mwanasheri Mkuu wa Kenya, pia zinahitaji
taasisi zote za kidini, kuwasilisha Katiba zao zenye taarifa za
misingi ya imani ya dini yao. Sheria hizo zinawahusu Maimamu,
Wachungaji pamoja na viongozi wengine wa kidini.
Kila taasisi ya kidini Kenya
inapaswa kuwa na Katiba yake, programu, matawi yake, shughuli za
kusaidia jamii na shughuli za kielimu zinazofanywa na dhehebu pamoja
na majina ya watu wanaosimamia shughuli hizo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni