Korea Kaskazini imesema wamefanikiwa
kufanya jaribio la bomu la hydrogen huku kukiwa na taarifa za
kuwepo kwa tetemeko karibu na eneo kuu la majaribio ya silaha za
nyuklia.
Chombo cha umma cha taifa hilo
kimetangaza majaribio hayo baada ya kutokea tetemeko la kipimo cha
alama 5.1 karibu na eneo la Punggye-ri.
Korea Kaskazini inasadikiwa kuwahi
kufanya majaribio matatu ya silaha za nyuklia aridhini siku za nyuma
katika eneo hilo tangu mwaka 2006.
Wananchi wa Korea Kaskazini wakifurahia taarifa za jaribio hilo
Kiongozi wa Korea Kaskazini akionekana akicheka
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni