Vindege vidogo vinavyoruka angani
kwa kuongozwa na remoti vimeelezwa kuwa vinaweza kuwa njia rahisi kwa
magaidi kuvitumia katika kuviboresha na kugeuzwa kuwa milipuko ya
angani.
Ripoti ya Wabobezi wa Matumizi ya
remoti nchini London, imependekeza watengenezaji wa ndege hizo
maarufu kama drone, waweke vidhibiti vya kutoweza kuruka katika
maeneo yasiyoruhusiwa.
Pia serikali ya Uingereza
imetahadharishwa kutokulegeza kamba kwa matukio ya kupokwa masafa ya
radio, na kuhimiza kuimarishwa kwa udhibiti wa utoaji leseni za
redio.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni