.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 3 Februari 2016

DK. SALIM KUZINDUA KITUO CHA UTAFITI NA MAFUNZO YA UYOGA CHA CHUO KIKUU CHA KAIRUKI



Katika kuadhimisha miaka 17 ya kumbukuzi ya mwaasisi wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert kairuki kuanzia tarehe 4 hadi 6 Feb ambayo itakuwa ni siku ya kilele.


Mh Dr Salmin Ahmed Salim ambaye pia ndio mkuu wa chuo hicho atazindua jengo la utafiti na mafunzo ya Uyoga lililopo huko Boko katika eneo la chuo hicho.

Sambamba na uzinduzi huo pia shughuli nyingine katika kumbukizo
hizo itakuwa ni pamoja na muhadhara kuhusu Uyoga utakaotolewa na
Profesa Keto Mshigeni ambaye ndiye  makamu mkuu wa chuo hicho na mwanasayansi aliyebobea katika tafiti za uyoga.


Pia hospital ya Kairuki it ataendesha zoezi maalum la upimaji na matibabu ya macho bila ya malipo kwa siku mbili mfululizo.

Pia patakuwepo matembezi ya hiara kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo yasaratani ya kizazi.

Aidha wanafunzi wa zamani wa chuo hicho waliopo Mwanza na mikoa ya kanda ya ziwa wataadhimisha kumbukizo hizo kwa kufanya zoezi la kupima afya bure kwa wakazi wa huko.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni