Bingwa wa zamani wa ngumi za uzito
wa juu duniani Muhammad Ali amepelekwa hospitali kutibiwa tatizo la
mfumo wa kupumua, msemaji wake amethibitisha.
Ali mwenye umri wa miaka 74,
anatibiwa na madaktari kama tahadhari, na imeelezewa kuwa yupo katika
hali nzuri kiasi.
Muhammad Ali alibainika kuugua
ugonjwa uitwao Parkinson mwaka 1984, baada ya kuachana na mchezo wa
ngumi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni