Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linalojishughulisha na matumizi ya mbolea Bara la Afrika anayesimamia eneo la Tanzania Dkt. Mshindo Msolla akitoa neno la shukrani baada ya ufunguzi wa warsha ya wadau wa mbolea kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla. Wa kwanza kushoto Mgeni rasmi ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka.
Mtaalamu wa Udongo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Dkt. Consolatha Mhaiki akichangia mada juu ya matumizi ya mbolea ni yanavyopaswa kuendana na aina ya udogo kwa uzalishaji bora wa mazao wakati wa warsha ya wadau wa mbolea iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada wakati wa warsha ya wadau wa mbolea iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka (katikati aliyekaa )akiwa picha ya pamoja na wadau wa mbolea mara baada ya kufungua warsha ya wadau ha oleo jijini Dar es salaam. (Picha na Eleuteri Mangi MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wadau wa mbolea wameaswa kuangalia namna ya kuboresha sheria na kanuni za kusimamia sekta ya mbolea kwa manufaa ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo ili kiwe na tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa mbolea uliofanyika leo jiji Dar es Slaam.
Dkt. Turuka amesema kuwa maeneo ya kuzingatiwa katika warsha hiyo ni pamoja na kuboresha sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya mbolea ili kuwezesha sekta binafsi kushiriki katika kuinua kilimo kwa manufaa ya Watanzania.
Gharama hizo zinahusisha kufanyiwa majaribio mbolea zinazotoka nje ya nchi kabla ya kuanza kutumiwa na wakulima ambapo majaribio hayo yanafanyika kwa misimu mitatu ya kilimo.
Maeneo mengine ya kurekebisha ni pamoja na mlolongo wa tozo ambazo zimekuwa zikitozwa kwenye mbolea inayoingizwa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linalojishughulisha na matumizi ya mbolea Bara la Afrika anayesimamia eneo la Tanzania Dkt. Mshindo Msolla amesema kuwa kazi kubwa waliyonayo wajumbe katika warsha hiyo ni kuhakikisha sheria na kanuni wanazozifanyia kazi zitasaidia kuboresha upatikanaji wa mbolea zenye ubora unaotakiwa kulingana na mahitaji ya wakulima na waipate kwa wakati.
“Wakulima hapa nchini wananufaika na huduma zetu ambazo tunatoa ikiwemo kuwaunganisha na mawakala wakubwa wa pembejeo na makampuni yanayozalisha au kuingiza mbolea nchini” alisema Dkt. Msolla.
Kuhusu hali ya upatikanaji wa mbolea nchini, Dkt. Msolla amesema kuwa shirika hilo linatoa huduma katika mikoa 12 nchini ambapo wapo mawakala 30 wanahudumia mawakala wadogo 500.
Mikoa hiyo ni Arusha,Kilimanjaro,Manyara, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Kigoma.
Mawakala hao msimu wa mwaka 2014/2015 wamefanikiwa kuuza kwa wakulima mbolea tani 60,000 na mbegu tani 3000 ambazo zimekuwa na manufaa katika kuhakikisha upatikanaji wa mazao ya chakula na biashara nchini.
Aidha, shirika hilo limefanikiwa kuwaunganisha wakulima na makampuni ya mbolea sita ikiwemo YARA, Extra Trading, Premium Agrochemical pamoja na Minjingu.
Vile vile, Dkt. Msolla amesema kuwa wakulima wamenufaika na kujengewa maghala 14 hadi sasa yameanza kutumika ambayo yanauwezo wa kuhifadhi tani 50,000 kwa wakati moja hatua ambayo inasaidia kusogeza huduma karibu na wakulima wanapozihitaji.
Dkt. Msolla amesema kuwa Shirika hilo lenye makao yake makuu Afrika Kusini linatoa huduma kwa sekta ya mbolea katika nchi mbalimbali Barani Afrika ikiwemo nchi tatu za kipaumbele ambazo ni Tanzania, Msumbiji na Ghana, nchi nyingine ambazo shirika hilo linafanya kazi ni Ethiopia, Senegal, Ivory Coast na Nigeria.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni