Mtoto wa kiume aliyepotea eneo la
msitu nchini Japan tangu jumamosi baada ya kuachwa na wazazi wake
kama adhabu, amepatikana akiwa hai.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka saba
aitwae, Yamato Tanooka, amekutwa kwenye kambi ya jeshi karibu na
Shikabe kaskazini mwa Hokkaido, kilomita chache kutoka alipoachwa na
wazazi wake.
Wazazi wake awali walisema mtoto
huyo amepotea, lakini baadaYe walikiri walimtelekeza kama adhabu kwa
kuwa ni mtukutu.
Mwanajeshi akionyesha magodoro aliyokuwa akilalia mtoto huyo kwenye kambi ya jeshi
Baba wa mtoto huyo Tamayuki Tanooka akiomba msamaha kwa kitendo chake cha ukatili dhidi ya mtoto wake
Muonekano wa kambi ya jeshi ambayo mtoto huyo alipatikana
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni