Viongozi wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Zanzibar wakifuatilia mashindano hayo yanayofanyika katika Masjid Loota Kiembesamaki Zanzibar na kuwashirikisha Vijana wa Umri mbali. Viongozi wa Kamati ya Kuhifadhi Qur-an wakiwa katikac Masjid Loota Kiembesamaki wakifuatilia Wanafunzi wakisoma Qur-an wakati wa mashindano hayo yalioandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Zanzibar. Washiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar wakiwa katika Masjid Loota wakisubiri zamu zao kushiriki mashindano hayo. yanayoshindanisha Wahifadhi Qur-an Juzuu 5.10,20 na 25. Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakifuatilia mashindano ya kuhifadhi Qur-an yanayofanyika katika Masjid Loota Kiembesamaki Unguja Wilaya ya Magharibi B Unguja. Majaji wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar wakiwa makini kufuatilia usomani wa Wanafunzi hao katika mashindano hayo. Watoa Aya za Qur-an kwa Washiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar wakitoa Aya kwa Washiriki hao. Mshinriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Juzuu 10 kutoka Zanzibar Mwanafunzi Khayyam Mohammed mwenye umri wa miaka 13. akisoma Qur-an wakati wa mashindano hayo yanayofanyika katika Masjid Loota Kiembesamaki leo 14/6/2016. Mwanafunzi kutoka Zanzibar Mussa Hamad mwenye umri wa miaka 9 akishiriki katika mashindano hayo ya kuhifadhi Juzuu 10, yanayofanyika katika Masjid Loota kiembesamaki Unguja Mshiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an kutoka Zanzibar Mwanafunzi Shakir Hamad Juma. akisoma Qur-an katika mashindano hayo yalioandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhi Qur-an Zanzibar. yaliowashirikisha Wanafunzi 27 Kutoka Zanzibar, Tanga, Pwani na Morogoro.
Imetayarishwa na Mtandao wa Zanzinews.com.
Email othmanmaulid@gmail.com – Zanzibar.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni