Bingwa
wa Olimpiki Usain Bolt, ameweka rekodi ya pili ya kukimbia kwa kasi
mwaka huu baada ya kushinda mbio za mita 100 nchini Jamaica licha ya
kuanza kwa kutetereka kidogo.
Bolt
alishinda mbio hizo kwa sekunde 9.88 katika michuano hiyo ya Racers
Grand Prix Jijini Kingston.
Baada
ya kuanza vibaya mbio hizo Bolt alimfikia Yohan Blake na kumpita na
kisha kumuacha Asafa Powell wakiwa katika mita 60 na kushinda
kiulaini mbio hizo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni