Marcos Alonso amefunga mara mbili
wakati Chelsea ikishinda Leicester kwa magoli 3-0 na kujikita
kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi saba, licha
ya Diego Costa kutocheza.
Chelsea walikuwa bila mfungaji wao
huyo magoli anayeongoza, baada ya kutofautiana na kocha kwenye
mazoezi kutokana na kutokuwa fiti kimchezo, na kunataarifa kapewa ofa
nono ya kuhamia ligi ya China.
Hata hivyo hali hiyo haikuwaathiri
na alikuwa Eden Hazard aliyemtengea pasi Alonso na kufunga ndani ya
dakika sita tu za mchezo, Mhispania huyo aliongeza la pili katika
kipindi cha pili na Pedro kukamilisha goli la tatu.
Mpira uliopigwa na Marco Alonso ukijaa wavuni na kuandika goli la kwanza
Pedro akiwa ameruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli la tatu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni