Dereva wa timu ya Ferrari Sebastian
Vettel amemshinda Lewis Hamilton wa Mercedes katika mbio za
langalanga za Australia Grand Prix.
Ushindi huo wa Vettel, ni wa kwanza
tangu ule wa Singapore GP, Septemba mwaka 2015 unaashiria kumalizika
kwa ubabe wa Mercedes, baada ya Ferrari kuja na gari zenye kasi.
Hamilton aliyekuwa akilalamikia
hitilafu ya matairi ya gari lake katika mbio hizo alimaliza wa pili
na mwenzake wa timu ya Mercedes Valtteris Bottas alikuwa wa tatu.
Dereva wa Ferrari Sebastian Vettel akiruka juu kwa furaha ya ushindi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni