Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akipokelewa na Mkuu wa Wilaya
ya Masasi, Seleman Mzee, wakati alipokuwa anawasili wilayani humo,
Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi. Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiongozwa na Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa (kulia), kuingia Gereza la Kilimo
na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi kwa ajili ya ukaguzi wa
Gereza hilo ambalo lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo
na ufugaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anamfafanulia jambo
mara baada ya kutoka ndani ya Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani
lililopo wilayani Masasi kwa ajili ya ukaguzi wa Gereza hilo ambalo
lina wafungwa ambao wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Mtwara (RPO), Ismail Mlawa, alipokuwa anatoa maelezo kuhusu
Gereza la Kilimo na Mifugo Lamajani lililopo wilayani Masasi. Gereza
hilo lina wafungwa zaidi ya 60 ambao wanafanya shughuli za kilimo na
ufugaji. Kikao hicho kilifanyika ofisi ya Mkuu wa Gereza hilo na
kuhudhuriwa na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo
vilivyo chini ya wizara yake pamoja na viongozi wa wilaya hiyo.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiiangalia moja ya nyumba za
askari magereza zilizopo jirani na Gereza la Kilimo na Mifugo
Lamajani wilayani Masasi, Mkoa wa Mtwara. Katikati ni Mkuu wa
Magereza Mkoa huo (RPO), Ismail Mlawa. Kushoto ni Ahmed Bakari, Kaimu
Mkuu wa Gereza hilo. Masauni alimaliza ziara yake ya mikoa ya kusini
kwa kutembelea Gereza hilo. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni