.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 2 Aprili 2017

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR, BALOZI SEIF KUZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA MKOANI KATAVI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa mara baada ya kupokea Taarifa ya Maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Kazi.Ajira, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzikbar Mh. Moudline Castico akimkabidhi Taarifa ya Maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baad ya kusomwa na Waziri mwenzake Mh. Jenista Muhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu Mh. Jenista Muhagama akitoa Taarifa ya kukamilika kwa maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Katavi.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha maandalizi ya sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru kilichofanyika katika Ukumbi wa Ikulu ndogo ya Mkoa wa Katavi hapo Mpanda.wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na OMPR - ZNZ)

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewasili Mkoani Katavi kwa ajili ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein.

Kwenye uwanja wa Ndege wa Mpanda Mkoani Katavi Balozi Seif aliyeambatana na Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud pamoja na Mkurugenzi Uratibu wa SMT na SMZ Nd. Khalid Bakar Amran alipokewa na Viongozi wa Serikali na vyama nvya Siasa.

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa katika Mikoa yote 31 ya Tanzania Bara na Zanzibar ambapo utachukuwa muda wa siku 195 hadi kuzimwa Rasmi ndani ya Mkoa Mjini Magharibi mnamo Tarehe 14 Oktoba mwaka 2017.

Akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya kazi ndani ya Mkoa wa Katavi wakati wa chakula cha Mchana mbele ya Mgeni rasmi na uzinduzi wa Mbio za Mbwenge Kitaifa, Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga alisema Mkoa huo uko salama hali inayowafanya Wananchi wake kuendelea na majukumu yao ya kila siku bila ya wasi wasi.

Meja General Raphael alisema hali ya upatikanaji wa chakula ambacho ndio jambo la msingi katika maisha ya kila siku ya Jamii inaridhisha kutokana na kuwepo kwa mazao ya nafaka kama Mpunga, Mtama na Ulezi yanayokadiriwa kufikia Tani Laki 873,661.

Alisema malengo ya kilimo kwa Mkoa wa Katavi katika mwaka 2017/ 2018 ni kulima Hekta Laki 646,847 za chakula licha ya wakulima wengi ndani ya Mkoa huo kukabiliwa na changamoto ufinyu wa pembejeo.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu Mh. Jenista Muhagama kwa Niaba ya Waziri mwenzake wa upande wa Zanzibar Mh. Moudline Castico alisema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru yamekamilika.

Waziri Jenista alisema pamoja na mabo mengine uzinduzi huo pia utajumuisha halaiki ya Vijana wapatao 800 watakaozipamba sherehe hizo zikiwemo pia ngoma za Utamaduni.

Akipokea Taarifa ya Maandalizi ya Sherehe hizo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushauri Umma wa Watanzania kuacha kuubeza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliopatikana kwa kuchanganya Damu.

Balozi Seif alisema Tarehe 26 Aprili mwaka 1964 ilikuwa ni siku ya kurasimisha tuu Muungano wa Tanzania ambao wadau wake tayari wameshaungana kwa takriban karne nyingi zilizopita nyuma.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/4/2017

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni