Mke wa aliyekuwa rais wa Marekani
Michelle Obama ametetea vikali jitihada zake za mlo wenye afya
mashuleni alizozianzisha wakati mumewe Barack Obama akiwa madarakani.
Akiongea katika mkutano wa Afya ya
Umma Jijini Washington, ameushambulia utawala wa rais Donald Trump
kwa kulegeza masharti ya virutubisho kwa milo ya mchana mashuleni.
Wakati akiwa Ikulu Michelle Obama
alianzisha kampeni ya "Let's Move", iliyokuwa ikihimiza
mazoezi, ulaji wa milo yenye afya kwa vijana na wanafunzi wa
Marekani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni