Timu ya Celtic imejuta kuifahamu
Paris St-Germain baada ya kupigwa magoli 5-0 katika Mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya huku Neymar akiongoza mauaji.
Mchezaji huyo ghali duniani alifunga
kiulani goli la kwanza na kuchangia goli la pili lililofungwa na
Kylian Mbappe.
Edinson Cavani akafunga la tatu kwa
mkwaju wa penati, Mikael Lustig akajifunga kisha tena Cavani akafunga
la tano.
Mshambuliaji Kylian Mbappe akifunga goli la pili la Paris St-Germain
Wakati huo huo Barcelona imeibuka na
ushindi nyumbani wa magoli 3-0 dhidi ya Juventus huku Lionel Messi
akifunga magoli mawili na Ivan Rakitic akifunga moja kwa shuti la
mbali.
Lionel Messi akimfunga kipa
Gianluigi Buffon hili likiwa ni goli lake la kwanza kuwahi kumfunga
kipa huyo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni