Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu akipata maelezo ya umbali wa upandaji mbegu wakati akizindua msimu wa kilimo 2017/18 ikiwa ni Sehemu ya kuwasihi wananchi kuanza kujiandaa kwani tayari wakati wa kuanza kilimo umekaribia.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturuakipanda mbegi wakati akizindua msimu wa kilimo 2017/18 ikiwa ni Sehemu ya kuwasihi wananchi kuanza kujiandaa kwani tayari wakati wa kuanza kilimo umekaribia.
Na Mathias Canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani
Singida Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu amezindua msimu wa kilimo
2017/18 ikiwa ni Sehemu ya kuwasihi wananchi kuanza kujiandaa kwani
tayari wakati wa kuanza kilimo umekaribia.
Katika uzinduzi huo uliofanyika
katika kijiji na kata ya Ihanja wilayani Ikungi Mhe Mtaturu pamoja na
mambo mengine lakini amewasihi kutumia vizuri mvua za mwanzo
kupandia.
Katika mkutano huo wa uzinduzi Mhe
Mtaturu pia ameanzisha utaratibu huo wa kuzindua msimu wa kilimo kila
mwaka ili kuwaandaa wakulima kuingia msimu mpya mapema ikiwemo
kuyakumbusha makampuni ya mbegu kuwafikishia wakulima mbegu kabla
mvua kuanza kunyesha.
Sambamba na utaratibu huo wa
kuzindua msimu wa kilimo kila mwaka pia kutakuwa na zoezi la kufanya
maonesho ya zana na teknolojia mbalimbali za kilimo ili wakulima
wapate muda wa kujifunza mbinu mpya za kilimo ili kuongeza uzalishaji
wa mazao ya chakula na biashara.
Mhe Mtaturu aliwaagiza maafisa ugani
kuwa na mashaba darasa na madaftari ya wakulima sambamba na
kuwaunganisha wakulima hao na makampuni ya mbegu ili waweze kupanda
mbegu bora zikiwemo zile zinazokomaa kwa muda mfupi.
Aliwakumbusha wakulima wote kulima
mazao ya chakula ili kuwa na usalama wa chakula ambapo aliyataja
mazao hayo ambayo yanastahili hali ya ukame kuwa ni pamoja na Mtama,
uwele, Mpunga, viazi lishe,viazi vitamu na mihogo.
Pia aliwataka wakulima kulima mazao
ya biashara ili kuwa na uchumi imara huku akitikisa msisitizo zaidi
katika mazao ya kipaumbele katika wilaya hiyo ambayo ni Korosho,
Pamba na Alizeti.
Mhe Mtaturu aliwahakikishia wananchi
kupanda mbegu mapema za korosho na dawa za kupulizia ili kuua
vijijidudu vinavyoshambulia.
Alisma kuwa tayari Wilaya ya Ikungi
imepokea Mbegu Tani 20 za Pamba ambazo zitaanza kusambazwa wiki ijayo
kwa wakulima waliojiandikisha.
Akisoma taarifa ya idara ya kilimo
kwa Mkuu wa Wilaya, Kaimu afisa kilimo Wilaya ya Ikungi Ndg Teendwa
Senkoro alieleza lengo la wilaya hiyo ku ni kulima hekta 124,038 za
mazao mbalimbali katika msimu wa mwaka 2017/18 na kuvuna tani 208,700
za mazao mbalimbali.
Mhe Mtaturu ametimiza ahadi yake ya
kuanzisha msimu wa kilimo aliyoahidi hivi karibuni wakati alipofanya
kikao kazi na wakuu wa Idara na Vitengo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe Ally Mwanga alimpongeza Mhe
Mtaturu kwa juhudi zake mbalimbali za kimaendeleo anazozifanya katika
Wilaya hiyo tangu ateuliwe kuhudumu katika nafasi hiyo.
Alisema kuwa waheshimiwa Madiwani na
Halmashauri wataendelea kumuunga mkono katika jitihada hozo ili
kuwasaidia wananchi kujiletea maendeleo.
MWISHO.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni