Viongozi wakuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Rais Wallace Karia na Makamu Rais
Michael Wambura wataongoza ujumbe wa shirikisho katika mazishi Kocha
wa zamani wa Taifa Stars, marehemu Joel Nkaya Bendera.
Bendera aliyefariki dunia Desemba 6,
mwaka huu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, atazikwa leo Jumapili
Desemba 10, 2017 makaburi ya Kijiji cha Manundu, Korogwe mkoani
Tanga.
Ujumbe huo pia utamjumuisha
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la TFF, Mhe. Mohammed Abdulaziz;
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi; Mwenyekiti wa Kamati ya
Ufundi, Vedastus Lufano pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa
Kanda ya 12 (Mikoa ya Tanga na Kilimanjaro), Khalid Mohammed.
Khalid Mohammed atakuwa na wenyeji
wengine ambao ni viongozi wa mpira wa miguu mkoa na wilaya za Tanga
ambao wataungana familia pamoja na waombolezaji wengine kumpumzisha
Mbunge huyo wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(1995 hadi 2005) katika Jimbo la Korogwe Mjini.
Mwili wa marehemu Bendera umeagwa
Jumamosi Desemba 9, mwaka huu asubuhi kwenye Viwanja vya Hospitali ya
Jeshi la Lugalo, Dar es Salaam.
Enzi zake Joel Nkaya Bendera
alifikia cheo cha Naibu Waziri Michezo mbali ya kuongoza mikoa ya
Morogoro na Manyara kwa cheo cha Mkuu wa mkoa.
Anakumbukwa zaidi kuwa sehemu ya
benchi la ufundi lenye mafanikio kuingoza timu ya soka ya Tanzania
kuiondoa Zambia na Tanzania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa
Huru ya Tanzania mwaka 1979.
Taifa Stars ilishinda bao 1-0 dhidi
ya KK Eleven ya Zambia (sasa Chipolopolo) na kuifanya Tanzania
kushiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo mikubwa Afrika kwa upande
wa timu za taifa iliyofanyika Nigeria. Taifa Stars haijafuzu tena
katika michuano hiyo.
Joel Bendera – ndiye aliyeiongoza
Simba kushinda mabao 5-0 dhidi ya Mufulira Wondereres huko Zambia
katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1979.
Ikumbukwe kwamba Simba ilifungwa
mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza ulifanyika Dar es Salaam.
Joel Bendera – ndiye aliyeiongoza
Coastal Union ya Tanga kutwaa ubingwa wa Bara na kucheza michuano ya
Afrika Mashariki na Kati na kuifikisha timu hiyo fainali. Wakati
akifanya kazi na hayati Zacharia Kinanda.
Joel Bendera – akiwa Naibu Waziri
Michezo, chini Waziri George Huruma Mkuchika ndiye aliyeihamaisha
Taifa Stars kucheza vema hadi kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa
ya kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), mwaka 2009.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni