.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 19 Aprili 2018

MSIINGIZE SIASA SUALA LA MABONDENI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa wajiepushe na tabia ya kuingiza siasa katika suala la kuwaondoa wananchi waishio mabondeni kwa kuwa jambo hilo linafanywa kwa maslahi ya wananchi wenyewe. 

Amesema wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha na mali zao kila yanapotokea mafuriko, hivyo ni vizuri kwa viongozi wakiwemo wabunge washirikiane na Serikali kuwahamasisha wakazi wote wa mabondeni wahame.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Aprili 19, 2018) wakati akijibu swali la mbunge wa Temeke, Bw. Abdallah Mtolea katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.

“Mara nyingi Serikali imekuwa ikiwataka wakazi ya maeneo ya mabondeni kuhama ila suala hilo limekuwa likikwamishwa na masuala ya kisiasa. “Wabunge ni mashahidi jambo hili linapoamuliwa, zinaingizwa siasa.”
Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wananchi walioathiriwa na maafa yaliyosababishwa na mafuriko zikiwemo familia za watu 12 waliofariki mkoani Dar es Salaam.

Katika swali lake, Bw Mtolea alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kudhibiti madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Dar es Salaam.

Mapema akijibu swali la Mbunge wa Nyang’hwale , Bw. Hussein Nassoro Waziri Mkuu alisema suala la kurejesha miundombinu iliyoharibika linashughulikiwa na kamati za maafa za mikoa na wilaya ambazo kwa sasa zinafanya tathmini ili kujua kiwango cha uharibifu na hatua gani zichukuliwe.

Bw. Nassoro alitaka kujua Serikali imejipangaje katika kurejesha miundombinu iliyoharibika kutokana na mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa wito wa wananchi kuhakikisha wanatumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao mbalimbali ya biashara na chakula. Kuhusu mazao ya biashara amesema Serikali itawasaidia kutafuta masoko.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Bi. Aida Khenani (Viti Maalumu), aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kuandaa masoko ya uhakika kwa mazao ya wakulima.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
ALHAMISI, APRILI 19, 2018.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni