.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 9 Agosti 2013

OPRAH WINFREY ALALAMIKA KUBAGULIWA JIJINI ZURICH


                                                                    Oprah Winfrey

Mtangazaji mahiri wa vipindi vya televisheni, Oprah Winfrey amesema alijikuta akikumbana na kitendo cha kibaguzi alipokuwa kwenye ziara yake hivi karibuni nchini Switzerland.

Winfrey amesema mmoja wa wahudumu katika duka moja kubwa la bidhaa Jijini Zurich alikataa kumuhudumia.

Winfrey, ambaye ni miongoni mwa wanawake matajiri duniani, aliambiwa na muhudumu huyo kuwa begi alilokuwa anataka kununua lilikuwa ni la bei ghali mno ambayo yeye hawezi kumudu kununua.

Madai hayo ya Winfrey ameyatoa kwenye kipindi cha televisheni, huku kukiwa na mvutano wa kisiasa katika baadhi ya miji ya Swiss juu ya kuwazuia wahamiaji kuingia kwenye baadhi ya maeneo ya huduma za umma.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni