Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta amewashukuru wakuu wa nchi za Afrika Mashariki kwa kujitolea kuwasaidia wakenya wakati wa tukio la kuungua moto uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta hapo jana.
Uhuru amesema marais wenzake wa Uganda,
Tanzania, Rwanda na Burundi ni miongoni mwa viongozi wa kwanza
kumtumia ujumbe wa kuwatia moyo wakenya baada ya sehemu ya uwanja huo
kuteketea kwa moto.
Rais Uhuru amesema hali hiyo
imemridhisha na kuonyesha kuwa ni kwa jinsi gani viongozi wa nchi
hizo walivyojidhatiti katika kuimarisha mahusiano na ushirikiano wa
karibu miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni