Timu ya soka ya Taifa ya Kenya Harambee Stars imefanikiwa kulitwa kombe la michuano ya kuwania kombe la Cecafa baada ya kuwalaza Sudan kwa mabao 2 - 0 katika mchezo uliokuwa mkali nawa kusisimua uliochezwa katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Ili kuhakikisha wanalibakiza kombe hilo nyumbani, iliwabidi Kenya kucheza jihadi kuwafunga Sudan ambayo ilikuwa ni moaj ya timu zilizocheza vyema katika michuano hiyo.
Mchezo huo ulishuhudiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Amolo Odinga, aliyekuwa Makamu wa Rais Kenya Kalonzo Musyoka na Rais wa Cecafa Leodger Tenga.
Kwa ushindi huo wa Harambee Stars wamenogesha sherehe zao za miaka 50 toka nchi hiyo ipate uhuru, sherehe ambazo zimefanyika hii leo nchini humo


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni