Maalim Gurumo ( katikati ) akifuatilia mazoezi hayo
Hafsa Kazinja, Edo Sanga, Juma Katundu na Jumbe wakijifua
Jumbe na Juma Katundu wakiteta jambo kuelekea tamasha la Gurumo kesho TCC Club
King Maluu na Yahaya wakipuliza mdomo wa bata " saxaphone "
Komandoo Hamza Kalala naye atakuwepo hiyo kesho TCC Club Chang'ombe
Mpiga drum Mashaka akifanya vitu vyake katika mazoezi hayo
Mazoezi hayo makali yalifanyika Amana Club ambako kwa wiki
nzima wanamuziki watakaoshiriki tamasha hilo wamekuwa wakikutana hapo na kupiga
mazoezi ya kufa mtu.
Baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na “Selina” utunzi wake
Gurumo kwa kushirikiana na marehemu Joseph Mulenga, “Barua kutoka kwa Mama”
uliotungwa na Cosmas Chidumule na “Gama” (Tshimanga Kalala Assossa).
Mratibu wa mazoezi hayo, Mzee Kassim Mapili alisema nyimbo
mbili zingine za Sikinde zitajulikana siku ya onyesho lakini akafichua kuwa
zitakuwa ni kati ya “Neema” (Chidumule), “Supu umeitia nazi” (Karama Legesu),
“Nachechemea” na “Isaya” (Hussein Jumbe).
Wasanii waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo
kumsindikiza Gurumo ni pamoja na Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein
Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni
Ali Yahaya na Boniface Kachala, Tshimanga Kalala Assossa, Shaaban Lendi na
Ibrahim Mwinchande.
Katika maendeleo mengine, Komandoo Hamza Kalala naye kwa
kushirikiana na wakongwe hao, amekamilisha mazoezi ya nyimbo mbili “Vicky” na
“Tumezaliwa wote Kijiji kimoja” ambazo zitapigwa Jumamosi kusindikiza tamasha
hilo.
Mkongwe Mzee Makassy nae katika tamasha hilo atashuka na
wimbo wake uliowahi kutamba sana “Anifa”.
Tamasha la Gurumo 53 ni maalum kwa ajili ya kuhitimisha
miaka 53 ya utumishi uliotukuka katika muziki wa dansi kwa Muhidin Maalim Gurumo
ambaye ametangaza rasmi kustaafu muziki.
Wasanii wengine wanaoshiriki mazoezi hayo ni Miraji
Shakashia, Hafsa Kazinja, Juma Katundu, Edo Sanga Majengo na King Maluu.
Burudani zingine zitakazokuwepo siku hiyo ni pamoja na bendi
za Msondo Ngoma Music Band, Talent Band, na Twanga Pepeta.








Hakuna maoni :
Chapisha Maoni