.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 12 Desemba 2013

WASHINDI WA SHINDANO LA UANDISHI WA INSHA NA UCHORAJI LILILOENDESHWA NA MULTCHOICE WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

SONY DSC 
Meneja Uhusiano wa Multchoice, Barbara Kambogi akiongea na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
Wadau walioudhuria kwenye hafla hiyo. SONY DSC 
Kushoto mwandishi wa habari wa Radio Times Adamu Husen.akiwa pamoja na wadau wengine kwenye hafla hiyo SONY DSC 
Kundi la THT.likitoa burudani wakati wa hafla hiyo. SONY DSC 
Mmoja wa washindi wa shindano la kuwasaka wanafunzi wakali wa uandishi wa insha na uchoraji nchini linaloendeshwa na Kampuni ya MultiChoice kila mwaka akipewa zawadi  SONY DSC SONY DSC 
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika hafla hiyo.

Fransisco Kibasa na Maghma Jammadas wameibuka washindi wa shindano la kuwasaka wanafunzi wakali wa uandishi wa insha na uchoraji nchini linaloendeshwa na Kampuni ya MultiChoice kila mwaka.
 
Meneja Uhusiano na kampuni hiyo, Barbara Kambogi aliwatangaza rasmi washindi katika hafla maalum ya wanahabari iliyofanyika jijini Dar es Salaam Disemba 12-2013.


“Kwa kutambua umuhimu wa elimu, MultiChoice imeamua kuwa bega kwa bega na Serikali kuhakikisha Watanzania wengi wananufaika na mfumo mpya wa elimu ambao ni wa kisayansi zaidi. Shule wanazotoka wanafunzi hawa tumezipatia pia zawadi maalum ya dishi na kisimbuzi ambacho kina channel maalum nane za elimu,” alisema Barbara.
 
Kibasa, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzunzumbe, Morogoro, aliibuka mshindi wa insha nzuri ya masuala ya satelaiti akifuatwa na Fabian Shayo kutoka shule hiyo pia. Kwa ushindi huo, Kibasa na wazazi wake watapata ofa ya kwenda Afrika Kusini mwakani kuangalia namna matangazo ya satelaiti yanavyorushwa.
 
Kwa upande wake, Maghma aliyeshinda uchoraji wa picha nzuri za satelaiti akifuatwa na Sanjma Joshi (wote kutoka Shule ya Sekondari Agha Khan Mzizima, Dar es Salaam), atasafiri na wazazi wake kwenda nchibni Ufaransa kuangalia namna roketi inavyorushwa angani.
 
Hafla hiyo iliyohudhuriwa na waharirir ma waandishi wa habari za michezo na burudani nchini, ilinogeshwa na wachezadansi wa Kundi la THT.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni