NSSF Tanzania imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na
wajasiriamali ili kuongeza zaidi elimu kwa wajasiriamali kuhusu Mfuko
huo wa Hifadhi ya Jamii pamoja na mafao yake yakiwemo ya matibabu,
uzazi, kuumia kazini na Mikopo ya SACCOS. Balozi alitoa pongezi kwa
Shirika hili pamoja na Taasisi za MKURABITA, TFDA, TanTRADE
zinazoshiriki kutoka Tanzania chini ya Wizara ya Afrika Mashariki na
Wizara ya Kazi.
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
limeonyesha tena njia kwa wadau wa sekta kwa kuvuka tena mipaka na
kueneza elimu kwa wajasiriamali wa Tanzania na Afrika Mashariki
washiriki wa maonesho maarufu yajulikanayo kama Jua Kali/ Nguvu Kazi
Exhibition ambayo hufanywa mara moja kwa mwaka katika nchi za umoja wa
Afrika ya Mashariki.
NSSF imeshiriki kwa mara
ya nne katika maonesho haya kwa nia mya kuongeza wigo wa wanachama
katika mfuko huo. Shirika hili linatoa mafao saba kwa mujibu wa tamko la
Kimataifa la Shirikisho la Kazi Duniani (ILO). Mafao haya yakiwemo ya
matibabu bure kwa Mwanachama na wategemezi wake, mafao ya Kuumia kazini,
mafao ya uzazi, na Mikopo kwa wanachama hutolewa wakati wakiwa kazini
na mafao ya muda mrefu kwa mtindo wa pensheni hutolewa pindi vigezo
vikikamilika. Pensheni husika ni ya Uzeeni, ya Ulemavu na ya Urithi.
Mafao
haya ya Muda mfupi hayapunguzi kiwango cha Pensheni itakayotolewa
itakapojiri. Meneja Kiongozi Uhusiano, Bi Eunice Chiume alinukuliwa
akieleza haya katika maonesho haya muhimu ya wajasiriamali.
NSSF
inawatangazia FURSA mbalimbali wadau wote wa sekta binafsi wakiwemo
Wajasiriamali na Wakulima zinazopatikana kwa kujiunga na uanachama wa
Shirika hili.
NSSF
pia imetoa FURSA kwa Watanzania wote waishio ughaibuni kujiunga na
Mifuko huu kwa mfumo wa WESTADI na kuwawezesha kupata mafao ya matibabu
kwa Wategemezi wanne waliopo Tanzania na usafirshaji wa mwili mwanachama
anapofariki nje ya nchi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni