.
.
.
.
.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga
|
TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.
mbani
NYUMBANI
HABARI
SIASA
MICHEZO
BURUDANI
TABASAMU
KIMATAIFA
Jumatatu, 16 Desemba 2013
RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA NELSON MANDELA, AONGEA KIJIJINI QUNU AFRIKA KUSINI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Dkt Dlamini Zuma kwa hotuba ya kusisimua aliyoitoa wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Kushoto ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda. Rais Kikwete alialikwa kuzungumzia sifa za mapambano ya ukombozi aliyoongoza Mzee Madiba ambapo Tanzania ndiyo ilikuwa ni nchi yake ya kwanza kusaidia mapambano yote ya ukombozi kusini mwa Afrika kwa kuwahifadhi na kuwapa misaada ya hali na mali wapigania ukombozi wake.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wageni wengine akitoka katika hema maalumu lililotumika kwa shughuli za mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Wa tatu kulia ni Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Uingereza Prince Charles.
PICHA NA IKULU
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni
Chapisho Jipya
Taarifa za zamani
Nyumbani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni ( Atom )
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni