.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 17 Desemba 2013

WAASI DR CONGO WAUA RAIA 20 KWA KUWAKATA KWA MAPANGA

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamesema zaidi ya watu 20, wakiwemo wanawake na watoto wameuwawa Mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wengi wao wameuwawa kwa kukatwa kwa mapanga siku ya Ijumaa na Jumamosi katika vijiji viwili Kaskazini mwa Kivu, ikiwemo wasichana wawili waliobakwa na kisha kukatwa vichwa.

Haijulikani ni nani hasa aliyeendesha shambulio hilo, lakini Umoja wa Mataifa umesema lazima wauaji hao waadhibiwe.

Kuna karibu vikundi 10 vya waasi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vinavyoendesha shughuli za uasi nchini humo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni