Majasusi wa
Marekani wameonya kuwa kundi la wapiganaji wa Somalia la al-Shabaab
huenda linapanga jaribio la kuishambulia Kenya.
Ulinzi
umeimarishwa na jitihada za kukabiliana na ugaidi nchini Kenya
zimeongezwa pamoja na nchi nyingine za Afrika Mashariki tangu tukio
la mauaji kwenye jengo la Westgate Jijini Nairobi Septemba mwaka
jana.
Hata hivyo Kamati
ya Intelijensia ya Marekani imesema nchi za Afrika Mashariki zitapata
muda mgumu kukabiliana na matukio mbalimbali ya majaribio ya
kushambuliwa na magaidi.
Kundi la
al-Shabaab pia limeelezwa kuwa linapanga mashambulio kwenye nchi za
Burundi, Djibouti, Ethiopia pamoja na Uganda kutokana na nchi hizo
kuwa na wanajeshi wake katika kikosi cha Umoja wa Afrika kilichopo
Somalia.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni