Bieber akishuka kwenye gari kuelekea Mahakamani
Mwanamziki Justin
Bieber ameendela kuandamwa na matukio, ambapo safari hii amefunguliwa
mashtaka ya kumpiga dereva wa gari la kifahari la kukodisha maarufu
kama limouseine, tukio ambalo ameripotiwa kulifanya mwezi DEsemba
mwaka uliopita nchini Canada.
Bieber mwenye umri
wa miaka 19 tu, amesababisha umati mkubwa wa mashabiki pamoja na
waandishi katika kituo cha polisi huko Jijini Toronto kuripoti kwa
ajili ya shitaka lake hili ambalo mwanasheria wake amesema kuwa hana
hatia.
Kwa mujibu wa
shtaka hili jipya, Bieber pamoja na mwenzake wameripotiwa kuhusika
katika kumtolea maneno makali pamoja na kumpiga kisogoni dereva huyo
siku ya tukio, na kesi hii itaanza kusikilizwa mahakamani tarehe 10
mwezi Machi.
Wakati hayo
yakijiri Rais Barack Obama wa Marekani anakabiliwa na shinikizo la
kumtaka kufikiria uwezekano wa kumtimua Marekani Bieber kutokana na
tabia yake mbaya ya kuvunja sheria.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni