Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe(kushoto), akimtabulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka(aliyevaa tai nyekundu) kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen, wakati Waziri Mkuu huyo alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), leo asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe akitoa
ufafanuzi wa namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa
Finland, Jyki Katainen(wa tatu kutoka kushoto) , wakati alipotembelea Mamlaka
hiyo leo asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka. Kulia
kwa Waziri Mkuu wa Finland ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na
kushoto kwa Waziri Mkuu huyo ni Waziri wa Niashati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni