.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 28 Januari 2014

TANAPA KUENDESHWA KWA MFUMO WA KIJESHI ILI KUDHIBITI UJANGILI

 Askari wapya waliomaliza mafunzo ya miezi mine katika Hifadhi ya Taifa Katavi wakipiga saluti kabla ya kuwasilisha risala yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi aliyekuwa mgeni rasmi Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo Sajini Taji Simon Mbunda akipokea zawadi yake iliyotolewa na wahitimu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi.


Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifunga rasmi mafunzo ya askari wapya 96 walioajiriwa na TANAPA na kuhudhuria mafunzo ya miezi minne katika Hifadhi ya Taifa Katavi mwishoni mwa wiki.

Kijazi alisema kuwa TANAPA imeanzisha utaratibu mpya ambapo sasa askari wanaoajiriwa na shirika kutoka katika Vyuo vya Wanyamapori vya Mweka na Pasiansi pamoja na wale wa kutoka Jeshi la Kujenga Taifa watalazimika kupitia mafunzo maalum yanayoandaliwa na shirika kwa ajili ya kuwawezesha waajiriwa wapya kufahamu mazingira halisi ya utendaji kazi katika eneo la uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi za Taifa.



Wahitimu wakionyesha igizo la namna ujangili unavyoendelea na mbinu za askari katika kukabiliana na vitendo hivyo vya ujangili katika maeneo ya hifadhi.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni