.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 3 Machi 2014

BOKO HARAM WAUWA RAIA WENGINE 39 KATIKA KIJIJI CHA MAINOK NCHINI NIGERIA

Wapiganaji wanaohisiwa kuwa ni wa kundi la Boko Haram wamewauwa kwa kuwapiga risasi watu 39 katika kijiji kimoja Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Washmbuliaji hao wamekiteketeza kijiji hicho cha Mainok kilichopo kilomita 50 Magharibi mwa Mji wa Maiduguri.

Tukio hilo limetokea jumamosi, ikiwa ni baada ya saa mbili kupita tangu kutokea kwa milipuko miwili iliyoua watu wapatao 50 huko Maiduguri.

Kundi la Boko Haram limekuwa likiendesha kampeni za miaka 4, kudai sheria za Kiislam Kaskazini mwa Nigeria.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni