Kiungo wa Roma na timu ya taifa ya
Italia Daniele De Rossi amefungiwa kucheza mechi tatu za Ligi ya
Serie A kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji mwenzake siku ya jumamosi.
De Rossi alikwaruzana na mchezaji wa
Inter Milan Mauro Icardi wakati wakigombea mpira katika mchezo ambao
uliisha kwa sare ya bao 1-1.
Kitendo hicho hakikuonwa na refa, hata
hivyo uongozi wa ligi ulifikia maamuzi hayo baada ya kuangalia
marudio ya tukio hilo kwenye TV.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni