.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 2 Machi 2014

LUPITA NYONG'O ATWAA TUZO NYINGINE KUELEKEA TUZO ZA OSCARS

                                     Lupita Nyong'o, Brad Pitt wakiwa na tuzo zao

Filamu ya 12 Years a Slave imepata ushindi mnono katika tuzo za Independent Spirit Awards kwa kutwaa tuzo tano, na kujiimarisha kuelekea katika tuzo za Oscars zitakazotolewa leo usiku.

Filamu hiyo ambayo inaelezea tukio la kihistoria, ilipata tuzo ya Muongozaji Bora Steve McQueen, Lupita Nyong'o akipata tuzo ya muigizaji msaidizi, pia tuzo ya filamu yenye mpangilio na uigizaji bora.

Kwa Lupita Nyong'o raia wa Kenya, tuzo hizo zimekuja wakati muafaka ambapo jana alikuwa akisherehekea kutimiza miaka 31 ya kuzaliwa kwake. 
                                           Lupita akiongea jambo na Angelina Jolie
         Angelina na Mumewe Brad Pitt wakiwa katika picha ya pamoja na Lupita

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni