Mshambuliaji wa Sunderland Fabio Borini akishangilia baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza
Yaya Toure akiifungia Manchester City bao la kusawazisha dhidi ya Sunderland
Nasri akiifungia timu yake bao la pili
Nahodha wa Manchester City Vicente Kompany akinyanyua juu kombe la Ligi " Capital One "
Timu ya soka ya Manchester City leo wametwaa kombe la Ligi " Capital One " baada ya kuifunga Sunderland mabao 3-1 katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Wembley. Sunderland ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Borini kunako dakika ya 10 kipindi cha kwanza, bao ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Man City kurekebisha makosa baada ya kufunga haraka haraka kupitia kwa Yaya Toure kunako dakika ya 55, Nasri akaongeza bao la pili dakika ya 56 na bao la 3 likifungwa na Navas dakika ya 90. Hili ni taji la kwanza kwa kocha Manuel Pellegrin tangu aanze kuifundisha Manchester City
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni