Vipindi vya televisheni vya shindano la Maisha Plus kuanza kuonyeshwa leo usiku katika kituo cha televisheni, TBC1.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Mratibu wa Mashindano
hayo, Masoud Ali ‘Kipanya’ alisema vipindi hivyo vitaonyesha hatua za awali
ambazo ni usaili na mpaka kupatikana kwa washiriki 30 waliobahatika kuingia
kijijini.
“Tutaanza kuwaonyesha kipindi chetu kuanzia leo hii saa nne
na dakika tano usiku, kipindi kitaanza kwa kuonyesha hatua za mwanzo kabisa za
mashindano haya,” alisema Kipanya.
Alifafanua akisema kuwa vipindi 10 vya mwanzo vitaonyesha
mchakato mzima wa upatikanaji wa vijana 18 kutoka Tanzania watakao ungana na
vijana wengine 12 kutoka Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi zitakazotoa washiriki
watatu kwa kila nchi.
Usaili wa mwaka huu ulikuwa tofauti na miaka mingine ambapo
orodha ya washiriki 40 ilitengenezwa na ikagawanywa katika makundi mawili
ambapo kundi la kwanza lilikwenda mkoani iringa kuishi kwenye vijiji vya huko
na kushiriki shughuli za kijamii.
Kundi la Pili litaenda visiwani Zanzibar ambalo pia
litashiriki utamaduni wa kila siku wa kimaisha wa visiwani humo ambapo ni
washiriki tisa tu katika kila kundi watachukuliwa na watachujwa kutokana na
jinsi walivyoyamudu maisha ya huko.
“Vijana wakiwa huko katika vijiji vya kweli watakuwa
wakishiriki shughuli za kilimo, usafi, za kiafya na nyinginezo kabla
hawajaingia katika kijiji cha Maisha Plus”, alifafanua Kipanya.
Baada ya kundi la kwanza na la pili kutoa washiriki tisa
kila kundi, washiriki 18 watakuwa wameshapatikana, na sasa nchi za zikishapata
washiriki wake 12, idadi ya washiriki 30 itaingia kijijini cha Maisha Plus
katikati ya mwezi huu

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni