Nchi ya Uganda itatuma kikosi maalum cha wanajeshi 410 kulinda Makazi ya Umoja wa Mataifa katika Jiji la Mogadishu nchini Somalia.
Msemaji wa Jeshi la Uganda Paddy Ankunda amesema kikosi hicho kitakuwa huru kushirikiana na maelfu ya vikosi vya kulinda amani vinavyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika kudhibiti vikundi vya wapiganaji.
Kundi la al-Shabab lenye mahusiano na al-Qaeda limeimarisha mno mashambulizi yake katika Mji wa Mogadishu, ambapo watu wapatao 12 waliuwawa Alhamisi katika tukio la bomu la kujitoa mhanga.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni