Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Italia Silvio
Berlusconi ameagizwa na mahakama moja ya Milan kujitolea kufanya kazi
za jamii katika nyumba ya kulelea wazee.
Hukumu hiyo inafuatia kutiwa hatiani
mwaka jana kwa kosa la kukwepa kulipa kodi katika ununuzi wa haki za
TV kupitia kampuni yake ya Mediaset mwaka 1990.
Wanasheria wa Berlusconi wamesema
wameridhishwa na hukumu hiyo kutoa fursa kwa mteja wao kuendelea
kujishughulisha na shughuli za kisiasa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni