.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 15 Aprili 2014

OFISI YA MBUNGE JIMBO LA UBUNGO YAZUNGUMZIA ATHARI ZA MAFURIKO JIMBONI HUMO

Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ubungo inapenda kutoa taarifa kuhusu athari za mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa na hatua ambazo imeendelea kuchukua kwa kushirikiana na mamlaka zingine katika wakati huu mgumu kwa wananchi wengi wa Dar es Salaam.

Kufuatia mafuriko hayo yaliyowakumba wakazi wa Dar es Salaam, wakiwemo wananchi wa Ubungo, Ofisi ya Mbunge Ubungo imekuwa karibu kusaidia, kufuatilia na kushirikiana na wananchi katika wakati huu mgumu, ambapo juzi msaidizi wa ofisi na madiwani kwa maelekezo ya mbunge, walishiriki maziko ya baadhi ya wahanga na kuwasilisha rambirambi kwa niaba yangu.

Aidha juzi na jana, timu ya mbunge iliendelea kutembelea maeneo yaliyoathirika. Baada ya kubaini hali ilivyo kutokana na athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali, tumeanza kuchukua hatua ya kurekebisha miundombinu;

Ambapo wasaidizi katika ofisi ya mbunge, kwa niaba yangu pamoja na wahandisi wa Manispaa ya Kinondoni wamekwenda Kata ya Msigani Mtaa wa Temboni, eneo la Msingwa ambako kivuko kimekatika na hakuna mawasiliano kati ya pande mbili.

Wakimaliza watakwenda Kata ya Makuburi katika mtaa wa Makoka ambako daraja limekatika na hivyo hakuna mawasiliano kati ya Tabata na Makoka.

Aidha, nakusudia kurejea jimboni kushirikiana kwa karibu zaidi na wananchi katika maafa yaliyojitokeza baada ya kufunguliwa kwa daraja lililokatiza mawasiliano Pwani kwenda Dar es Salaam.


Imetolewa leo Jumanne, Aprili 15, 2014 na;

John John Mnyika (MB)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni