Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini
Oscar Pistorius leo ameiambia mahakama kuwa alivunjika moyo baada ya
kuona mwili wa mpenzi wake Reeva Steenkamp aliyemuua kwa kumpiga
risasi.
Kauli hiyo ya Pistorius ameitoa baada
ya upande wa mashtaka kumaliza kumhoji kwa siku tano, mahojiano
ambayo yalimfanya aangue kilio mara kwa mara.
Pistorius amekanusha shtaka la mauaji,
ambapo amekuwa anasisitiza kuwa alidhania kuwa kunamtu kavamia nyumba
yake.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni