Bondia Manny
Pacquiao amemdunda Timothy Bradley kwa pointi na kushinda mkanda wa
WBO wa uzito wa welterweight Jijini Las Vegas, Nchini Marekani.
Mfilipino Pacquiao
ambaye alipoteza mchezo wake dhidi ya Mmarekani Bradley katika
pambano lililogubikwa na utata mwaka 2012 , safari hii alitangazwa
mshindi na majaji wote watatu.
Akiongelea ushindi
huo wa usiku wa jana Pacquiao amesema amethibitisha kuwa safari yake
ya ubondia itaendelea kuwa njema, huku Bradley akisema amejaribu
lakini ndio hivyo amepoteza mchezo huo dhidi bondia bora duniani.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni